Ogiek in the Mau Forest, Kenya

Haki za Ardhi za Jamii asili Tanzania na Kenya – Athari za mikakati ya kufungua madai mahakamani na uhalali wa kuwawezesha kisheria

MRG hivi karibuni imeanzisha tathmini ya madai na uwezeshaji wa kisheria wake katika programu zake ambazo imetekelezwa kwa jamii chache zinanazohujumiwa na makabila asili katika Africa ya mashariki kwa miaka kumi na tano iliyopita. Tathmimi iligundua kwamba shughuli hizi ni vifaa vya nguvu ambavyo vinatoa nafasi katika kuunganisha jamii na harakati za mashindano yao ya kupata haki na kufanya uamuzi ambao una athari za hakika na kweli katika haki za kijumla. Thathmini hii Iliangazia kesi za Waendoroisi na Waogieki kutoka Kenya na Wamaasai kutoka Tanzania. Matokeo haya ya mikakatai ya kufungua madai mahakamani katika programu hizi yalipelekea kuwa na mafaniko makubwa kwa jumla na yalihamatishwa kwa kutoa vidokezo muhimu kwamba masomo makuu yanaweza kutolewa kutoka kwake ambayo yanaweza kutekelezwa kwa kufanya shughuli sawa na hii siku kzijazo.

Matokeo yaliyowasilishwa katika ripoti kamili yalitokana na maoni ya moja kwa moja kutoka kwa jamii husika. Vipengeee msingi kutoka kwa tathmini hii vimewekwa kwa muhstasari hapa here huku listi kuu ya hitimisho na mapendekezo zinapatikana katika ripoti.

1. Sababu za kawaidia katika muktadha ni mizizi katika kufungua madai mahakamani na kuweka mikakati

Sehemu ya adhari ya mikakati ya kufungua madai mahakamani Afrika mashariki inatokana na kuimarisha hoja katika muktadha wa: Jamii asili wanaotafuta fidia ya mashamba waliyopoteza. Waendorori, Waogieki na Wamaasai wana historia sawa za ukiukaji waliopata wa haki za kibinaadam. Haki zao za mashamba na raslimali zao hazijaliwi na nguvu za wakolonina pamoja na sababu zingine za nje ziilzopelekea kunyakuliwa kwa mashamba yao kwa nguvu, kufukuzwa kutaka mashamba yao bila ya kushauriana au kutopewa fidia ya kutosha. Madai ya kisheria ilikuwa jitihada ya kutafuta suluhisho ya migogoro iliyokita mizizi kihistoria kwa nchi zote mbili, jamii na hali ya kisiasa ambayo imekuwa ikipinga kutambuliwa kwa haki za mashamba za jamii asili kulingana na sheria ya kimataifa

Historia ya kushirikiana kisheria kutoka na jamii pia ni sababu ya kawaida. Jamii hizi zote tatu ziliijia MRG zikiiomba msaada baada ya miaka mingi bila mafanikio ya kuweza kushirikisha mfumo wa sheria wa mataifa yote matatu yaliyokuwa hayatambui haki zao. Miktadha hii ya kawaida kupitana kwa haki za kibinaadam kwa viwango vilivyopelekea kuwa na jukwaa la nguvu la muongozo wa jamii katiaka mikakati ya kisheria na kufungua mashtaka mahakamani.

2. Matokeo: Mradi wa mda mrefu

Mfumo wa haki za kibinaadam katika sehemu hii ya Afrika mashariki umetoa uamuzi ukipendelea jamii asili na kutoa amri ya kurudisha ya kurejeshwa na kuchochewa kwa mpango imara wa kuwapa msaada kutekeleza hatua muhimu zilizopatikana kwa jamiii ni muhimu. Kwa mambo ya urekebishaji na kupata matokeo bora ni sababu muhimu, kushinda kesi ya sehemu hii ilikuwa mwanzo tu wa mchakato wa kupigania haki zao.

Kwa jamii zote tatu, sababu kuu za madai ya kisheria zimekuwa chache na kutekelezwa kwake ni changamoto kuu. Matarajio ya ufanisi wa utekelezaji wake haujafaulu kwa mda mrefu kutokana na ukosefu wa rfedha za msaada na raslimali za binadamu kwa kitaifa na mashirika yasiyo ya serikali, pamoja na haki za kibinadamu na taratibu za idara za serikali ambazo ni husika kwa utekelezaji mwema, kwa hiyo misaada zaidi inahitajika.

3. Athari za kisheria : swala linaloendelea

Athari za mikakati ya madai kwa mfumo wa sheria nchini Kenya na Tanzania si sambamba kama ilivyotarajiwa huku wezeshaji kisheria wa jamii hizi ni hakika kwamba Mahakama nchini Kenya na Tanzania hazijaunga mkono kikamilifu sheria ya kimataifa kwa haki za Jamii asili. Mafunzo ya majaji na marejistra yaliyofanyika Tanzania yalionyesha dhahiri umuhimu wa shughuli kama hizi ili kuhamasisha waamuzi kuhusu haki za jamii asili Afrika na kimataifa.

Madai ni sehemu moja ya utetezi wa mikakati inayolenga sheria ya kitaifa pamoja na taaluma ya sheria kuwa ya makini kabisa na haki za jamii asili kama inavyolingana na sheria ya kimataifa. Kutokana na mtazamo huu, madai ya kisheria yanayofunguliwa mahakamani ni chombo cha nguvu cha kutetea madadiliko na athari za madai yanopata kuonekana katika jamii, sehemu zingine mbalimbali na hata katika viwango vya kimataifa, huku kuchangia kwa jamii asili katika mashirika nchini Kenya na Tanzania na kutoka MRG na kanda zingine kulingana na falsafa za sheria Afrika ni Jambo la ajabu.

4. Athari katika Jamii: Umuhimu wa Kuezeshwa kisheria na athari zake katika jamii

Katika harakati za madai ya mchakato wa sheria, mabadiliko makubwa na muhumu

yameonekana. Ripoti zilizozopokelewa kuhusu uimarishahji wa jamii, jamii zinahisi haki. Kupewa nguvu kisheria na umoja katika kung’ang’ania haki ni jambo la mda mrefu.

Kuna mabadiliko madogo katika mtazamo na tabia katika sehemu zingine za jamii, kama jamii jirani, serikali za mikoa na mashirika ya habari pia zimeripotiwa kutokana na matokeo ya sheri na haki za kibinaadamu na shughuli zingine katika madai ya kufungua mashataka mahakamani, ingawa hali hii ya mambo imebaki kuwa tete.

Ikizingatiwa kuwa hawapati msaada wa vifaa na mabadiliko ya kusheria. Pia, katika kesi ya Kenya na Tanzania, kuna mambo Fulani ambayo yalielezewa kuwa ya wasiwasi na jamaii Kuwa kuleta madai na kufungua kesi mahakamani yanaweza kuchangia ongezeko la fadhaa na mvutano na vita pale hali ya jamii na siasa si thabiti. Hatua za uajibikaji zinahitajika na programu ya madai na operesheni katika hali hizi ni lazima kuongezwa nguvu na usalama na kuchekecha hatua na kuchanganua hatari ili kuzuia vita pamoja na kupata nafasi ya ufadhili na jinsi ya kutatua kesi za vita

5. Utetezi na mikakati na muungano katika siku zijazo

Uzoefu wa kufungua madai katika mahakama kwa mfumo wa haki za Kibinaadam Afrika unaonyesha kuwa ni wazi kuna mafanikio katika jukwaa hili la mabadiliko. Ingawa ni mchakato utakaochukuwa mda mrefu matumizi ya mitambo ya sheria za haki za kibinaadam za Afrika inawezekana kuendelea kutoa matokeo ya kudumu na yenye uendeleazi kwa haki za jamii asili.

Katika kesi ya haki za mashamba za jamii asili, kutunza mazingira ni hoja nzito ambayo inafaa utetezi mwingine kukiwa na mtazamo wa kuleta mafanikio na ubadilishaji wa sheria. Jukumu la Jamii asili kwenye kutunza na kuhifadhi mazingira kwa wakati mwingi huwekwa kwa sayansi ya falsa ya sheria ya kimataifa lakini serikali bado hazijatilia maanani hoja hii na kwa hivyo juhudi zaidi zinahitajika katika upande huu ili kupelekea kuwa na matokeo ya kweli.

Kama MRG, inavyoangazia ushirikiano wao Afrika na mahamali pengine popote, tathmini hii inaangazia kwamba kuangazia vitu vya kawaida kwa undani kunaweza kuipa nguvu mikakati ya kufungua madai mahakamani. Juhudi zenye nguvu na namna mbali mbali katika utekelezaji wa sheria kupitia waamuzi ni muhimu. Wafadhlili wanafaa kuweka ahadi kuendelea kufadhili kwa kina na pia kwa muda mrefu ili kuendelea kutoa msaada unaohitajika ka ajili ya kupata mabadiliko. Tathmini ya jamii katika mradi huu pamoja na ushirikiano mkubwa na MRG, utaendelea kupitia ushirikishi wa wanawake, vijana na wazee and mwishowe msaada kwa mikakati mingine ya shughulili zitakazokuwa zinaendelea sambamba na madai yanayowasiliswhwa kortini